Misingi Ya BIBLIA
Study 9: Ushindi Wa Yesu
Ushindi Wa Yesu | Damu Ya Yesu | Kutoa Dhabihu Kwa Ajili Yetu Na Kwa Ajili YaNafsi Yake Mwenyewe | Yesu Ni Mwakilishi Wetu. | Yesu Na Torati Ya Musa | Sabato | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Sanamu ndogo ya Yesu Msalabani, Je? Yesu alizaliwa December 25?) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 29: Je? Yesu alizaliwa December 25?

Kosa lingine kubwa la ukristo wa watu wengi ni kuhusu siku ya kuzaliwa Yesu. Wachungaji walikuwa wamelala kondeni na mifugo yao wakati wa kuzaliwa Kristo (Luka 2:8); hawakufanya hivi wakati wa Krismasi, majira ya kipupwe. Kristo aliishi miaka 331/2 na kisha alikufa kwenye sikukuu ya Paska, ambao ni wakati wa kufufuka. Basi inapasa kuwa alizaliwa miezi sita upande mwingine wa Pasaka, yaani karibu mwezi wa September/October.

Tarehe 25 Disemba ilikuwa ni sikukuu ya Kipagani huko Ulaya kabla ya Ukristo kuingia. Taarifa ya matendo ya Mitume inayo habari jinsi gani Wakristo wa kweli waliteswa vibaya mno na wapagani kwa sababu ya imani zao. Mara kwa mara mitume walionya kuwa kwa sababu hii, Wakristo wengine walitafuta imani za kipagani, ili kuwezesha dini yao iwe ya kupendeza zaidi mbele ya wapagani waliowazunguka (k.m Mdo 20:30, 1 Yoh. 2:18; 2Thes 2:3; 2Pet 2:2-3). Kuichagua tarehe 25 Disemba kuwa sikukuu ya Kikristo huu ni mfano mkubwa. Miti ya Krisimasi n.k yote yaweza kufuatiliwa kurudi nyuma hadi kwenye kanuni za ibada ya kipagani zilizotendwa tarehe 25 Disemba.

Kwa sababu hii Wakristo wa kweli wasisherekee kuzaliwa kwa Kristo tarehe 25 Disemba. Kwa matendo, waamini wa kweli watatumia siku za mapumziko ya watu wote, k.m krisimasi, kuabudu pamoja popote iwezekanavyo.