Misingi Ya BIBLIA
Study 9: Ushindi Wa Yesu
Ushindi Wa Yesu | Damu Ya Yesu | Kutoa Dhabihu Kwa Ajili Yetu Na Kwa Ajili YaNafsi Yake Mwenyewe | Yesu Ni Mwakilishi Wetu. | Yesu Na Torati Ya Musa | Sabato | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Sanamu ndogo ya Yesu Msalabani, Je? Yesu alizaliwa December 25?) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 28: Sanamu ndogo ya Yesu Msalabani

Kwa upana imeaminika kwa Wakristo ya kwamba Yesu Kristo aliuwawa msalabani. Walakini neno la Kiyunani ‘stauros’, ambalo kwa kawaida limetafsiriwa ‘msalaba’ katika Biblia, maana yake hasa ni mti ambao umesimikwa ardhini kama nguzo au mti wa kuchonga. Hakika, alama ya sanamu ya Yesu Kristo amepigiliwa msalabani imeelekea kuwa chanzo chake ni kwenye upagani. Inafaa ya kwamba Kristo na mikono yake na viganja viliinuliwa juu ya kichwa chake kuliko kwamba aliitandaza kwa mfano wa Yesu msalabani, kwa kuwa mikono iliyonyooshwa kuelekea juu ni ishara ya ahadi ya Mungu imethibitishwa (Ezek. 10:5,6,13; 36:7; 47:14), pamoja na sala (Omb 2:19;1 Tim 2:8; 2 Nyak 6 12,13; Zab 28:2), ambayo Kristo alijirikisha msalabani (Ebra 5:7). Alisema kama vile nyoka wa shaba alivyoinuliwa kwenye mti Israel walipokuwa jagwani, basi atainuliwa wazi mbele za watu muda wake wa kufa; hivyo alijumuisha ‘msalaba’ na mti (Yohana 3:14).

Kanisa Katholiki limefungasha fumbo kubwa lenye ushawishi kuelekea msalabani. Wazo hili halina usaidizi kabisa na Biblia; limesababisha sanamu ya Yesu msalabani kuwa wazo la bahati njema, ishara ya kuonekana kwamba Mungu yu pamoja nasi. Watu wamefikiri ya kwamba kuvaa msalaba shingoni au kila mara kuonyesha alama ya msalaba, Mungu atakuwa pamoja nao. Hii ni ishara tupu; nguvu ya kweli ya msalaba ni kwetu sisi kuungana na mauti ya Kristo kwa kuamini na kubatizwa, kuliko kurudia mfano wa kuonekana na msalaba. Kwa kweli ni vyepesi kufanya la pili kuliko la kwanza.