Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 23: Nimeshuka kutoka Mbinguni

"Maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na aupaye ulimwengu uhai ..... kwani nimeshuka kutoka mbinguni"(Yn. 6: 33, 38 B.H. N). Tafsiri toka Biblia Habari njema sio U.V.

Maneno haya, na mengine kama hayo, yametumika vibaya kusaidia wazo potofu kwamba Yesu alikuwako mbinguni kabla ya yeye kuzaliwa. Ingawa hivyo vipengele vifuatavyo inabidi vitazamwe:

  1. Wanao amini katika Utatu na Mungu wanachukua maneno haya kuwa ni halisi ili kuthibitisha maana yao. Lakini, kama tutaelewa kwa maneno jinsi yalivyo, basi hii ina maana kwamba kwa njia isiyoeleweka Yesu mwenyewe alielea na kushuka kutoka angani kuja chini. Sio tu kwamba Biblia imekuwa kimya kuhusu jambo hili, bali msemo wa kuwa Yesu alizaliwa mtoto mchanga katika tumbo la Mariamu unafanywa kuwa hauna maana. Yohana 6: 60 unaeleza mafundisha yanayohusu mana kuwa ni neno"gumu, ni nani awezaye kufahamu"(tafsiri ya Moffatt): yaani, tunahitaji kuelewa kuwa ni lugha ya kimfano iliyotumika.

  2. Katika Yohana 6, Yesu anaeleza jinsi gani mana ilikuwa ni mfano wake mwenyewe. Mana ilitoka kwa Mungu katika maana ya kuwa Mungu ndiye aliyehusika kuiumba duniani; katika umbile haikupeperuka toka juu kwa Mungu mbinguni na kufika chini. Basi Kristo kuja toka mbinguni ieleweke vivyo hivyo; aliumbwa duniani, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ndani ya tumbo la Mariamu (Luk. 1: 35).

  3. Yesu anasema kwamba"chakula (mkate) nitakachotoa ni mwili wangu"(Yn.6: 51) Makundi yanayoamini Utatu yanadai kwamba ilikuwa ni sehemu ya'Mungu’ huyu Yesu aliyekuja toka mbinguni. Lakini Yesu anasema kwamba ulikuwa"Mwili"wake uliokuwa chakula kilichoshuka toka mbinguni. Vivyo hivyo Yesu anajumuisha chakula toka mbinguni na mwili wake mwenyewe kuwa'Mwana wa Adamu"(Yn. 6: 62), Sio'Mungu Mwana’.

  4. Katika fungu hili la maneno kwa Yohana 6 kuna ushahidi mwingi wa kwamba Yesu hakuwa sawa na Mungu."Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi"(Yn. 6: 57) mstari unaonyeshaYesu na Mungu hawashiriki usawa wa pamoja; ukweli ni kwamba "nami ni hai kwa Baba"(Yn. 6: 57) ni shida kuishi pamoja milele ambako hao wafundishao utatu husema.

  5. Inabidi kuuliza, Ni lini na jinsi gani Yesu'alishuka' toka mbinguni? Wanaofundisha wazo la utatu hutumia mstari huu katika Yohana 6 ili"Kuthibitisha"kwamba Yesu alikuja toka mbinguni alipozaliwa. Lakini Yesu anajisema mwenyewe kuwa"kile kishukacho kutoka mbinguni"(mstari 33, 50) kana kwamba ni jambo linaloendelea. Akizungumzia Yesu ni kipawa cha Mungu, Kristo alisema"Baba yangu anawapa ninyi chakula"cha kweli kutoka mbinguni (mst. 32 U.V). Wakati Yesu akisema maneno haya, tayari alikuwa'amekuja’ kwa maana halisi kwa kuwa alikuwa ametumwa na Mungu. Kwa sababu hii, vile vile aliweza kusema kwa tendo lililopita tayari - yaani lilikwisha fanyika wakati uliopita:"Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichushuka kutoka mbinguni"(mst. 51). Bali pia anasema kuhusu'kushuka’ akiwa chakula kutoka mbinguni kwa namna ya kifo chake msalabani:"Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu"(mst. 51). Basi tunaye hapa Yesu akisema tayari'ameshuka’ toka mbinguni, na anaendelea kushuka, bado inambidi ashuke kwenda chini kwa kifo chake msalabani. Ukweli huu pekee uthibitishe kwamba'Kushuka’ kunamtaja Mungu akijifunua mwenyewe, kuliko kutaja tu kuzaliwa kwa Kristo. Kwa nguvu hili linathibitisha yote ya Agano la Kale yamtajayo Mungu'kushuka’ yakiwa na maana moja tu. Hivyo Mungu akaona mateso ya watu wake katika nchi ya Misri, naye'akashuka’ kuwaokoa kwa mkono wa Musa. Ameuona utumwa wetu wa dhambi basi'ameshuka’ au amejidhihirisha yeye mwenyewe, kwa kumtuma Yesu mwenye maana kama Musa ili atuongoze toka utumwani.


  Back
Home
Next