Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

7.1 Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale

Somo la 3 limeeleza jinsi gani lengo la Mungu kuwaokoa watu liliwekwa katikati kumzunguka pande zote Yesu Kristo. Ahadi alizotoa kwa Hawa, Ibrahimu na Daudi zote zilimsema Yesu kuwa ni mtoto wao halisi. Kwa kweli, Agano lote la Kale lilionyesha mbele na kutabiri kumhusu Kristo. Sheria ya Musa, ambayo Israeli iliwapasa waitii kabla ya wakati wa Kristo, mara nyingi ilionyesha mbele kuja kwa Yesu:"Torati ilikuwa ni kiongozi kutuleta kwa Kristo," (Gal. 3:24).Basi kwenye siku kuu ya Pasaka, mwana kondoo asiye na kasoro ilibidi achinjwe (Kut. 12: 3-6); hii inamaanisha dhabihu ya Yesu,"mwana kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu" (Yn. 1: 29; 1 Kor.5:7). Hali ya kutokuwa na doa ambayo ilitakiwa kwa wanyama wote wanaotolewa kuwa dhabihu ilitabiri jambo lililokuwa mbele la sifa njema kamili ya Yesu (Kut. 12:5; 1Pet. 1: 19).

Zaburi zote na vitabu vya manabii vya Agano la Kale kuna unabii usiohesabika kumhusu Masihi atakavyokuwa. Hasa walilenga kwa kuelezea jinsi atakavyo kufa. Wayahudi kukataa kukubali wazo la Masihi anaye kufa laweza tu kwa sababu ya wao kutoangalia unabii huu, baadhi yake sasa unatolewa:

Unabii ulio katika Agano la Kale

Umetimilika kwa Kristo

"Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha ?"(Zaburi 22: 1)

Haya yalikuwa kabisa ni maneno ya Yesu palemsalabani (Math. 27: 46).

"Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu. wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakatikisa vichwa vyao; Husema, umtegemee (yaani, alimtegemea) Bwana; na amponye; na amwokoe sasa, maana apendezwa naye"(Zaburi 22: 6 -8).

Israeli walimdharau Yesunao walimdhihaki (Luk. 23:35 8:53); walitikisa vichwa vyao (Math.27:39), walisema haya maneno alipokuwa msalabani (Math. 27:43).

"…. Ulimi wangu waambatana na taya zangu; wamenizuia mikono na miguu"(Zab. 22:15,16)

Huu ulitimia Kristo)alipokuwa na kiu msalabani (Yn.19:28). Kuzuiwa mikono na miguu ni tendo la kusulubiwa ambalo limetajwa.

"Wanagawanya nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura"(Zab. 22: 18)

Utimilifu kabisa wa huu unapatikana katika Mathayo. 27:35.

Ujue ya kwamba Zaburi 22: 22 ni bayana imenukuliwa kumhusu Yesu katika Waebrania 2:12.

"Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, namsikwao kwa wana wa mama yangu Maana wivu wa nyumba yako umenila"(Zab. 69: 8,9)

Huu vema unaelezea mawazo.ya Kristo kuvunjwa urafiki toka kwa Wayahudi ndugu zake na jamaa yake mwnyewe (Yn. 7:3 -5; Math12: 47 -49). Huu umenukuliwa Yn. 2:17.

"Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki"(Zab. 69:21).

Jambo hili lilitokea wakati Kristo akiwa msalabani (Math. 27:34).

Sura nzima ya Isaya 53 ni unabii wa kustaajabisha wa kifo cha Kristo na ufufuo, kila msitari ulikuwa unatimia bila kosa. Mifano miwili tu inatolewa: -

"Kama mwana-Kondoo apelekwaye machinjoni…. Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam hakufunua kinywa chake"(Isa. 53:9)

Kristo, Mwana kondoo wa Mungu, alikaa kimya wakati wa hukumu yake (Math. 27:12,14)

Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya, na pamoja na matajiri katika kufa kwake"(Isa. 53:9)

Yesu alisulubiwa pamoja na wahalifu (Math. 27:38), bali alizikwa ndani ya kaburi la mtu tajiri(Math. 27:57-60)

Ni ajabu ndogo ya kwamba Agano Jipya linatukumbusha ya kuwa"Torati na Manabii"wa Agano la Kale ndio msingi wetu kumweka Kristo (Mdo. 26:22; 28: 23; Rum 1: 2,3; 16: 25,26). Yesu mwenyewe alitahadhalisha kwamba kama hatumwelewi vema"Musa na Manabii", hatuwezi kumfahamu (Luk. 16:31; Yn. 5:46, 47).

Ikiwa Torati ya Musa ilionyesha mbele kwa Kristo, nao manabii walitabiri habari zake, unakuwa ni ushahidi wa kutosha kwamba Yesu kuishi katika mwili kabla ya kuzaliwa. Mafundisho potofu ya kwamba"aliishi akiwa na mwili Kristo kabla ya kuzaliwa yanafanya ahadi zilizorudiwa -rudiwa kwamba atakuwa mzao (mtoto) wa Hawa, Abrahamu, na Daudi ni upuuzi. Kama alikuwa tayari anaishi mbinguni wakati hizi ahadi zinatolewa, Mungu angekuwa amekosea kuwaahidi watu hawa kupata mtoto atakayekuwa masihi. Ukoo wa Yesu, ulioandikwa kwa Mathayo 1 na Luka 3, unaonyesha jinsi Yesu alikuwa na mfuatano wa mababu ambao mlolongo wao unarudi nyuma hadi kwa wote ambao Mungu alifanya nao ahadi.

Ahadi aliyoahidiwa Daudi kuhusu Kristo inakanusha kuishi na mwili wake wakati ahadi ilipofanywa:"Nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako ….Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa mwanangu"(2 Sam. 7: 12,14), Fahamu wakati ujao ulivyotumika hapa. Kwa kuwa Mungu atakuwa Baba ya Kristo, haiwezekani kwamba mwana wa Mungu tayari alikuwa akiishi wakati ule hapo ahadi zilipokuwa zinafanywa. Ikiwa mzao wako"atatoka viunoni mwako"inaonyesha ya kuwa alikuwa mtoto halisi mwenye mwili wa Daudi."Bwana amemwapia Daudi neno la kweli …. Baadhi ya wazao wa mwili wako nitawaweka katika kiti chako cha enzi"(Zab. 132:11).

Sulemani alikuwa wa kwanza kutimiza ahadi, lakini tayari kwa kuwa alikuwa akiishi wakati hizi ahadi zinatolewa (2 Sam. 5: 14), utimizwaji mkuu wa ahadi hii kuhusu Daudi kuwa na mzao wa mwili atakaye kuwa ni mwana wa Mungu, anatajwa Kristo (Luk. 1: 31-33)."Nitamchipushia Daudi chipukizi la haki"(Yer. 23:5) - yaani, Masihi.

Kama huu msemo wa kutaja wakati ujao katika unabii mwingine kuhusu Kristo umetumika."Mimi nitawaondokeshea (Israeli) nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe (Musa)"(Kum. 3:22,23, ambao unabainisha "nabii"kuwa ni Yesu."Bikira (Mariamu) atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake"Emmanueli"(Isa. 7:14). Huu kwa utimilifu ni wazi Kristo alipozaliwa. (Math. 1: 23).


  Back
Home
Next