Misingi Ya BIBLIA
Somo La 1: Mungu
Uwepo wa Mungu | Nafsi yake Mungu | Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake | Malaika | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Mungu ni roho" (Yohana 4:24), "Matumizi ya jina la Mungu", "Ufunuo wa Mungu") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 3: "Ufunuo wa Mungu"

Kinachufuata sio rahisi kukishika chote wakati tunaposoma kwanza,lakini umuhimu wa jambo tunalolizungumzia litakuwa dhahiri kadri masomo yake yanavyosonga mbele. Tunajumuisha kwenye maana hii ili uliache somo hili lote Msingi wa Biblia ukisha pimwa wenye ufunuo kuhusu Mungu mwenyewe.

Jina la Mungu laweza kuchukuliwa na yeyote ambaye amemchagua kujifunua au kujidhihirisha yeye mwenyewe. Hivyo watu na Malaika sawa sawa na Yesu huweza kuchukua jina la Mungu. Hili ni jambo la muhimu ambalo linatufunulia mengi ya Biblia. Hata mwana anaweza kuchukua jina la Baba; ana mambo mamoja na Baba yake, anaweza kuwa na jina lile lile la kwanza- lakini si mmoja na kuwa mtu yeye yule kama Baba. Kwa njia hiyo hiyo mwakilishi wa kundi anaweza kusema kwa niaba ya kundi, anaweza kumpigia mtu wa kwenye shughuli na kusema, Haloo ! hapa ni wakulima, Si Bw. Wakulima, bali anachukua jina lao kwa kuwa anafanya kazi kwa niaba yao. Basi hiyo hata kwa Yesu ilikuwa hivyo.

MALAIKA HUCHUKUA JINA LA MUNGU

Tumeambiwa katika Kutoka 23:20,21 ya kwamba Mungu aliwaambia watu wa Israeli kuwa Malaika atawatangulia mbele yao;'Jina langu limo ndani yake’, waliambiwa. Jina lake Mungu ni'Yahweh’. Basi, Malaika huchukua jina la Yahweh, na hivi anaweza kuitwa Yahweh, au BWANA kwa herufi kubwa neno BWANA linatokana na Yahweh, katika Biblia UV ya Kiswahili ni sehemu moja tu Zaburi 89:8 utakuta neno

YAHU = YAHWEH. Tumeambiwa kuwa katika kutoka 33:20 Mtu hataniona uso akaishi; lakini katika Kutoka 33:11 tunasoma kwamba "BWANA"(Yahweh) alinena na Musa uso kwa uso, kama mtu anaposema na rafiki yake - Yaani kirafiki. Hakuwa ni BWANA, Yahweh mwenyewe alikuwepo, aliyenena na Musa uso kwa uso, Kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kumwona Mungu yeye mwenyewe. Alikuwa ni Malaika aliyechukua jina la Mungu ndiye aliye fanya hivyo, na tunasoma habari za BWANA akisema uso kwa uso na Musa wakati hasa ni Malaika aliyefanya hivyo (Mdo. 7:30-33).

Ipo mifano mingine mingi ya maneno' Mungu' na BWANA ikitaja Malaika wakiwa Mungu mwenyewe. Mfano mmoja ulio wazi ni Mwa. 1: 26 "Mungu (Malaika) akisema, na tufanye mtu kwa mfano wetu"

WATU NA JINA LA MUNGU

Moja ya maneno ambayo yanayosaidia sana katika kuelezea yote haya ni katika Yohana 10:34-36. Hapa Wayahudi walifanya kosa ambalo wengi wanaoitwa'Wakristo’ wanafanya leo. Walidhani kuwa Yesu alikuwa anasema kuwa yeye ni Mungu mwenyewe. Yesu alisahihisha kwa kusema "Haija andikwa katika sheria yenu, nimesema Ninyi ni Mungu ? Ikiwa aliwaita Miungu ….. inakuwaje mimi …." Mnaniambia ninakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni mwana wa Mungu ? Yesu kwa kweli alikuwa anasema 'Katika Agano la Kale watu waliitwa Miungu; mimi nasema ni mwana wa Mungu, basi imekuwaje mnaudhika sana? Yesu kwa kweli alikuwa ananukuu toka Zab 82 mahali ambapo waamuzi wa Israeli waliitwa'Miungu’.

Kama ilivyoonekana, Jina kamili la Mungu katika Kiebrania ni 'Yahweh Elohim’ likiwa na maana, Nitadhihirika katika kundi la wenye nguvu. Waamini wa kweli ni wale wengi wenye nguvu katika maana ndogo ya maisha haya nao watakuwa na nguvu tele kwenye Ufalme. Kwa mlinganisho huu wote umeonyeshwa kwa Isa. 64:4 na 1 Kor.2:9.

"Watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikumwona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye" Paulo ananukuu mstari huu katika 1 Kor.2:9-10: Imeandikwa, Jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Fungu la maneno katika Isa. 64:4 linasema hakuna hata mmoja isipokuwa Mungu anaweza kufahamu mambo aliyowaandalia waamini; Lakini 1Kor. 2:10 mstari unasema kwamba mambo hayo yamefunuliwa kwetu, hivyo katika maana sisi ni "Mungu": sio Mungu mwenyewe katika utu, bali ufunuo wa Mungu kwa matokeo kuwa tumebatizwa katika jina lake na kujua Ukweli.

YESU NA JINA LA MUNGU

Sio jambo la kushangaza kwamba Yesu, Ikiwa ni mwana wa Mungu na ufunuo wake mkuu kwa watu, Pia naye atachukua jina la Mungu. Aliweza kusema "Nimekuja katika jina la Baba yangu" (Yoh.5:43). Kwa utii wake, Yesu alipaa kwenda mbinguni, naye Mungu akampa jina lipitalo majina - Jina la Yahweh, la Mungu mwenyewe

(Fil. 2:9).basi hii ndiyo sababu tunasoma Yesu anasema katika Uf 3:12 "Nami nitaandika juu yake (Mwamini) Jina la Mungu wangu……na jina langu mwenyewe, lile jpya"Kumbuka Yesu alitoa kitabu cha Ufunuo miaka mingi baada ya kupaa kwenda mbinguni na akiisha kupewa jina la Mungu, kama ilivyoelezwa katika Wafilipi 2:9.

Hivyo anaweza kuliita jina la Mungu "Jina langu Jipya"; Jina ambalo hivi karibuni alipewa. Sasa tunaweza kuelewa vema Isaya 9:6, mahali ambapo kuhusu yeye tumeambiwa "Jina lake (Ujue kuwa) utaitwa, Mshauri wa Ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, …." Huu ni Unabii wa kwamba Yesu atachukua majina yote ya Mungu ya kwamba atakuwa ni ufunuo wote wa Mungu kwetu.Na ndivyo kwa maana hii aliitwa "Emmanueli" maana yake 'Mungu ni pamoja nasi’ ingawa yeye hakuwa Mungu.


  Back
Home
Next