Misingi Ya BIBLIA
Mwishoni Mwa Kitabu
1: Maelezo Mafupi Ya Msingi Wa Mafunzo Ya Biblia | 2: Tabia Yetu Kujifunza Biblia | 3: Kristo Amekaribia Kurudi | 4: Haki Ya Mungu

Mwishoni Mwa Kitabu 3: Kristo Amekaribia Kurudi

Maneno ya Kristo katika Math 24:36 yanaweka wazi kuwa hatujua kamwe wakati hasa wa kuja tena mara ya pili: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake" (linganisha Mdo 1:7). Ingawa hivyo, wafuasi walipomwuliza Yesu, "Nayo ni nini dalili ya kuja kwako?" (Math 24:3), hakuwajibu kwamba swali lao lilikuwa gumu kulijibu. Hakika aliwapa ishara ambazo zitaonekana katika ulimwengu kabla ya kurudi. Yesu asingaliwapa hizi isipokuwa alikusudia kizazi kinachoishi kabla ya kurudi kiweze kwa upana kutambua ya kuwa kwa kweli kinaishi katika "siku za mwisho". Ipo sababu nzuri ya kutumaini na kuamini ya kwamba tumo kwenye siku hizo za mwisho sana.

DALILI ZINAONYESHA KURUDI TENA KRISTO

Katika Mathayo 24 na Luka 21, Yesu alinena wakati hapo

  1. Kutakuwa na manabii waongo wakidai kuwa ni Kristo
  2. Vita na vurugu vitaenea duniani
  3. "Kutakuwa na njaa, magonjwa na matetemeko"
  4. Kukengeuka toka kwenye kweli kutakuwepo.
  5. Watu watavunjika mioyo kwa hofu ya hali itakayakuwapo duniani, "kwa kutazamia yatakayo upata ulimwengu" (Luka 21:26).

Ni kweli kwamba siku zote ulimwengu umekabiliwa na matatizo yanayongezeka ya aina hii. Ni bayana Yesu alijua ukweli huu; kwa hiyo ni halali kusadiki kuwa alikuwa anataja kwa wakati hapo shida hizi zitakapokuwa kubwa mno hata kutishia kuiharibu sayari. Hapawezi kuwepo shaka, kwa mtazamaji wa makini ulimwengu, kwa kweli hii ndiyo hali iliyopo. Matumaini ya ajabu ya hali ya mwanadamu na kutopenda kwake kufikiri vilivyopo kukabili nafasi yetu, kunafanya iwe shida kwetu kufahamu hii hali ilivyo.

Ifuatayo ni sehemu ndogo tu ya ushahidi unaopatikana ambao unaonyesha jinsi maneno ya Kristo sasa yanatimilika:

1). Kwa karibu kila bara kuna mkondo usiogeuka wa watu waongo wenye kadhia ya kuwa na ufunuo na maarifa maalum na madhehebu yanayosema yanauwezo wa kuponya na ya kuwa yana vipawa ambayo yanawavuta watu kuwafuata.

2). Ifuatayo ni habari ya hesabu inayoonyesha jinsi matatizo yasiyotazamiwa ya vita yakiongezeka - mbali ya juhudi za wanadamu pamoja kama kuyazuia:

Karne Vita na majeruhi, waliouawa
(mamilioni)
Idadi ya vita kuu
ya 17 3.3 ?
ya 18 5.0 ?
ya 19 5.5 ?
1900-1945 40.5 19
1945-1975 50.7 119

(Mtoa taarifa: Kitivo cha Uangalizi wa mapigano, Chuo kikuu cha London)

3). Shida kubwa ya njaa na magonjwa ya kuambukiza yanajulikana vema kwetu sote. UKIMWI kwa ukubwa na maradhi yanayo ambukiza kwa kuenea ulimwengu pote ambao umejulikana. Mbali na maneno ya Yesu katika Mathayo 24 na Luka 21, kuna mafungu kadhaa mengine ya maneno yanayo jumuisha matetemeko ya ardhi na kurudi Kristo: Isaya 2:19-22; Ezek . 38:20; Yoel 3:16; Hagai 2:7; Zek 14:3,4. Kwa kadri ya kuangalia matetemeko ya hivi karibuni yakitokea kwenye maeneo yasiyotegemewa pamoja na hasara isiyotazamiwa ya matokeo ya hasara ya maisha, yaweza kudokeza ya kwamba tunaanza kuona utimilifu wa dalili ya tetemeko vilevile. Habari ya idadi ifuatayo kuhusu matetemeko, iliyotolewa na idara ya ndani ya Serikali ya Amerika vilevile ni ya maana:

Mwaka    Taarifa ya
Idadi ya

Mitetemeko
1948 620
1949 1152
1950 2023
1964 5154
1965 6686
1976 7180

4). Kupungua mkazo juu ya umuhimu wa ukubwa kufuata Biblia ili kupata mafunzo ya kweli umesababisha ukengeufu mkubwa toka kweli ya Biblia. Umoja wa elimu ya binadamu kwa gharama yote ambayo sasa imeenea katika jamii imeongeza kasi katika maendeleo haya.

5). Mazoea yanayoongeza kasi ya kutoangalia hali ya kweli na kupenda anasa yanayoonekana katika kila jamii ya sasa ni ushahidi wa kutosha wa hofu ya mwanadamu kwa ajili ya wakati ujao. Wanasayansi, wachumi na wataalam wa mimea na wanyama na mazingira yao wote wanakubali ya kuwa ulimwengu hauwezi kuendelea kama ulivyo sasa. Kuondoa na kuharibu mali za asili, uchafuzi wa hewa, bahari na utando wa ozoni angani, pamoja na vitisho vya mambukizo na maangamizi ya nyuklia yote yanaonyesha uangamizo wa ulimwengu wa sasa. (ona Tumeacha kitambo kidogo tuchokiandika sehemu ya 9). Kwa kutunza hiyo ahadi, Mungu itampasa kumtuma Yesu kubadili upesi na kueleweka hii sayari kwa kusimamisha Ufalme wa Mungu juu yake.

KUANZISHWA TENA TAIFA LA ISRAELI

Yesu alikamilisha kwa kutosheleza vema orodha yake ya ishara ya maelezo dhahiri: "Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi" (Lk 21:27). Aya inayofuata inawapatia faraja pekee wale ambao wamekwisha batizwa nao wanaishi katika dhamiri njema mbele za Mungu: "Basi mambo hayo yaanzapo kutokea (sasa!), changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu; kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia" (Lk 21:28).

Kisha Yesu aliongeza habari ya ziada kwa unabii huu wa kuja mara ya pili, kwa namna ya mfano wenye kuongoa unaohusu mtini: "Utazameni mtini na miti mingine yote; wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yameisha kuwa karibu, nanyi kadhalika, mwonapo hayo yaanzapo kutokea, tambueni ya kwamba Ufalme wa Mungu u karibu (na kwa hiyo kuja mara ya pili. Amini nawaambieni, kizazi hiki hakitapita mpaka hayo yote yatimie" (Lk 21:29-32). Kwa uchunguzi wetu kuchipuka kwa mimea, tuna akili ya ujuzi wa kujua kiangazi na kipupwe au kubadilika majira kunakuja; vivyo "mtini" uanzapo kuchipuka, tuwe na fahamu ya jinsi hii ya kuwa kizazi chetu kitaona kuja kwa pili Bwana. Mtini ni ishara ya Biblia inayotaja taifa la Israeli (Yoeli 1:7; Hosea 9:10; Yeremia 24:2 linganisha Ezek. 36:8). Hii ishara maalum ya kurudi Kristo mara ya pili inataja basi kuanzishwa tena taifa la Israeli (‘kuchipuka’) kwa njia nyingine. Matukio ya upesi yaliyo pamoja na kukua kwa Israeli tangu kuanzishwa tena kuwa taifa katika mwaka 1948 hakika inabidi kuwa ya maana katika fungu hili la maneno.

WAKATI UJAO ISRAELI KUVAMIWA

Unabii mwingi wa Biblia unatoa maelezo ya kuvamiwa Israeli, uvamizi mkubwa utakao tokea wakati wa kurudi Kristo. Zaburi 83 inatoa habari ya mataifa yakiizingira Israeli na kuwa muungano wa pamoja dhidi yake yakisema "Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, na jina la Israeli halitakumbukwa tena"……. Na tutamlaki makao ya Mungu" (Zab. 83:4,5,12). Tambua ya kuwa huu ni uvamizi wa siku za mwisho kwa Israeli likiwa taifa. Kuanzishwa kwake kuliopo lilivyo taifa ni muhimu basi kama utangulizi wa uvamizi huu wa mwisho juu ya taifa. Wasomaji wa Biblia walikuwa wakitabiri kuanzishwa tena taifa miaka mingi kabla ya kutokea (tazama kwa mfano, John Thomas Elps Israeli, kitabu ambacho kilichapishwa kwanza mwaka 1848. Kazi inayochapishwa tena inapatikana kwa wachapishaji). Msimamo wa wavamizi wa Israeli umeelezwa katika Zab. 83 hasa ni mashindano ya waarabu, majirani wa Israeli wa leo. Siku zote wanaeleza uchungu wa chuki yao isiyotulizika kwa Israeli, wakidai mji wa Yerusalemu ni wao mji wa Uislamu. Zaburi inaendelea kueleza jinsi shambulio lao litakavyoisha kwa haraka Mungu atakapo ingilia kati, na matokeo yakiwa kusimikwa Ufalme wake utakao enea ulimwenguni pote (Zab 83: 13-18).

Unabii mwingine unatoa maelezo ya mfululizo wa matokeo yaya haya: kuvamiwa Israeli na Waarabu, na toka jeshi la Kaskazini na maadui wengine, na kusababisha Mungu kuingilia kati kwa njia ya Kristo akiwa amerudi kusimamisha ufalme (k.m Ezekiel mlango wa 38-40; Dan. 11:40-45). Kusoma kwa kina unabii kama huu unafanya sehemu muhimu ya makuzi yetu kiroho haraka baada ya ubatizo. Zekaria 14:2-4 ni kati ya ulowazi sana: "Nitakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu, na huo mji utapigwa (linganisha Lk :21:24), nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri…… hapo ndipo atakapotokea BWANA, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita (Yaani, kwa ajabu ataingilia kati mambo ya ulimwengu kama alivyowahi kufanya zamani). Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa Mashariki"

Uvamizi huu mkubwa kwa Israeli unaweza kutokea muda wote sasa, zana za vita zinaongezeka kwa kasi na matendo ya kisiasa. Sio dhana njema kuwaza kuwa tutangojea hadi uvamizi ndipo tuitikie Injili, tukikumbuka maneno ya Paulo: "wasemapo kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla…." (1 Thes 5:1-3). Kamwe hatutaweza kujua siku hasa atakaporudi Kristo, tunachojua tu ni kwamba siku imejumuishwa na uvamizi kwa Israeli toka Kasakzini, na ya kwamba uvamizi huu unaonekana kana kwamba utatokea mapema. Yawezekana utakuwepo uvamizi mwingine juu ya Israeli kabla ya huo ulionenwa kwenye unabii ambao tumeona; lakini wasomi wa Biblia wataendelea kuangalia kwa makini nafasi ya Israeli. Tunajua ya kwamba hatimaye Mungu ataingilia kwa njia ya Kristo miguu yake kusimama juu ya mlima wa Mizeituni. Ilikuwa toka mlima u huu ambao Kristo alipaa mbinguni, na kwa huo atarudi. "Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomuona akienda zake mbinguni", Malaika waliwaambia wanafunzi waliposimama juu ya mlima huo, wakikaza macho Bwana wao akipaa juu (Mdo 1:9-12).

Fahamu zetu inabidi tuziwianishe kwa jinsi Kristo alivyokaribia kurudi. Unabii kuhusu matukio ya ulimwengu karibu kurudi kwake umetolewa kwa upana ili kuimarisha imani ya hao ambao tayari wamejitia wenyewe katika Kristo kwa kubatizwa. Ingawa hivyo, ulinganifu dhahiri kati yao na hali ya ulimwengu uliopo ni hakika hauna budi kuwa zaidi kuliko kuvutia kwa hao ambao bado kuchukua hatua, na vile vile unabii utasaidia imani yetu katika Neno la Mungu la kutegemewa lenye kuvuviwa. Utii wetu haupaswi kusukumwa na akili ya uoga wa kuwa kuja kwa pili kumekaribia. Wale tu wapendao kweli "kufunuliwa kwake" (2 Tim 4:8) watapokea thawabu. Hata hivyo, ni nafasi yetu ya kuangalia upesi, tunaishi ukingoni kabisa mwa wakati na yatakayotokea kwa wanadamu kama tujuavyo, kamwe isikome kukazwa kwetu kila siku ambayo tunaishi.


  Back
Home
Next