Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.3.3 Sala

Moja ya majaribu makubwa yanayozuka toka kumjua Mungu wa kweli ni kuwa mbinafsi kiroho. Tunaweza kutosheka mno na uhusiano wetu tulionao na Mungu, kujishughulisha sana katika kusoma kwetu wenyewe Biblia na kwa kiroho, hata tunaweza kuacha kushirikiana mambo haya na wengine-pande mbili ndugu waaminio na ulimwengu unaotuzunguka. Neno la Mungu na Injili ya kweli inayopatikana ndani yake, imelinganishwa na nuru au taa iwakayo gizani (Zab 119:105; Mithali 4:18). Yesu alieleza wazi kwamba hakuna mtu aliye na nuru hii halafu akaiweka chini ya kiango bali huionyesha kwa watu wote (Math 5:15). "Ninyi ni nuru ya ulimwengu" kwa sababu ya kubatizwa katika Kristo, "aliye nuru ya ulimwengu" (Math 5:14; Yoh 8:12). "Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima" Yesu aliongea (Mathayo 5:14).

Kama kweli tunaishi maisha ya kulingana na Injili ya kweli tunayoifahamu, ‘utakatifu’ wetu utakuwa dhahiri kwa hayo tuishiyo. Hatutaweza kuugeuza ukweli ambao umetufanya ‘tujitenge’ kwa ajili ya tumaini la Ufalme, na vile vile ‘tumejitenga toka’ njia za watu wa ulimwengu.

Kwa njia yenye busara, tutataka kushirikiana maarifa yetu ya kweli ya Mungu na wale wote tunaokutana nao: mazungumzo yakigeukia kuzunguka mambo ya Kiroho; kujadili mafundisho ya washirika wa makanisa mengine, tukigawa vitabu kidogo vyenye mafunzo ya dini, na hata kuweka matangazo madogo kwenye magazeti ya mahali maalum, haya yote ni njia ya kutuwezesha nuru yetu iangaze. Hatuta waza ya kwamba tunaweza kuiacha kazi ya kushuhudia kwa waamini wengine; sisi kila mmoja anao wajibu wa kufanya kazi ya kushuhudia neno. Kwa kulinganisha, Kristadelfiani wametunga hatua za kwanza chache zenye kipimo kikubwa cha kuhubiri mbali kabisa na makundi mengine. Sisi sote kila mtu mmoja mmoja, anaweza kufanya anacho weza, zaidi kwa gharama zetu wenyewe.

Moja ya njia zenye mafanikio zaidi katika kuhubiri ni kwa kueleza imani yetu kwenye jamii yetu na hao ambao kwa karibu sana tunakutana nao. Hao walio na mapenzi wasio katika imani ni wazi wataeleza imani yao kwao, ingawa mara hii kazi ikiisha fanywa sio busara kuendelea kuzusha hizi habari au kutoa mkazo wowote juu yao. Waongofu waliosongwa si ambao Mungu awataka. Jukumu letu ni kuishuhudia kweli pasipo jambo la kuchelewa kuhusu idadi ya wanaoitikia. Tuna wajibu mkubwa wa kushuhudia huku (Ezek 3:17-21); kama Kristo anakuja wakati tukiwa na uhai wetu "watu wawili watakuwa shambani; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa" (Luka 17:36). Hakika itakuwa ajabu ikiwa hatukusema mbele ya jamii yetu na wafanyakazi wenzetu juu ya kuja mara ya pili Bwana wetu linapokea hili.


  Back
Home
Next