Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

4.9 Kuzimu

Wazo la kuzimu kwa watu wengi ni mahala pa adhabu kwa'roho zisizopatwa na kifo’ za wabaya moja kwa moja baada ya kufa, au mahala pa kuteswa wale ambao watakataliwa. Ni tendo letu la kusadikisha kwamba Biblia inafundisha kuwa kuzimu ni kaburi, mahali watu wote wanakwenda wakifa.

Ni neno lisilotumika sana katika misemo ya watu, awali katika Kiebrania neno'Sheol’ limetafsiriwa'hell’ kwa kiingereza. kwa hiyo Biblia ya kiswahili ilipoandikwa tafsiri toka kiingereza neno liliandikwa'Kuzimu’ likiwa na maana'mahala pa kuzika wafu’ Leo watu wametoa habari zinazotofautiana na Biblia inavyoelezea kuhusu neno kuzimu. Biblia yetu ya kiswahili hapa Afrika Mashariki ni U.V ikiwa na maana kuwa ni tafsiri tofauti -tofauti toka Biblia mbali mbali za kiingereza ambazo ni K.J.V, R.S.V, R V n.k sasa hivi Biblia zilizopo kwa kiswahili ni U.V na Biblia habari njema kiswahili cha kisasa kwa kifupi (B.H.N) mifano michache ambayo katika Biblia hili neno'Kuzimu’ limetafsiriwa'kaburi’ linafanya wazo la watu wengi kutofaa kuhusu kuzimu kuwa ni mahala pa ziwa la moto na kuteswa wabaya ni: -

"E e BWANA, …….. wasio haki wanyamaze kuzimu" (Zab. 31:17).

"Bali BWANA ataikomboa nafsi yangu, atanitoa mikononi mwa kuzimu - Kaburi (Zab. 49:15) yaani nafsi ya Daudi au mwili atafufuliwa toka kaburini, au kuzimu’.

Imani ya kuwa kuzimu ni sehemu ya kuadhibiwa wabaya mahala ambapo hawawezi kuepuka haiwezi kupatana na hii; mtu mwenye haki anaweza kwenda kuzimu (Kaburini) na kutoka tena. Hosea 13:14 anathibitisha hivi: "Nitawakomboa (watu wa Mungu) na nguvu za kaburi (kuzimu); nitawaokoa na mauti" mstari huu umenukuliwa katika 1 Kor. 15: 55 unahusu ufufuo Kristo akirudi. vivyo hivyo katika maono ya ufufuo wa pili (ona somo la 5. 5) "mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwemo ndani yake" (Uf. 20:13). Tazama mfano kati ya mauti yaani, Kaburi, na kuzimu (pia ona zaburi 6:5).Maneno ya hana katika 1 Sam. 2:6 yapo wazi kabisa: "BWANA huua naye hufanya kuwa hai (Kwa njia ya ufufuo): hushusha hata kuzimuni (kaburini), tena huleta juu".Kwa kuwa'kuzimu’ ni kaburi itegemewe kwamba wenye haki wataokolewa kutoka hilo kwa njia ya kufufuliwa kwao kupata uzima wa milele. Hivi inawezekana kabisa kuingia'Kuzimu’ au kaburini, na baadae kuliacha kwa njia ya ufufuo. Mfano mkubwa ni huo wa Yesu, ambaye roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukupata kuoza’ (mdo. 2:31).wa sababu alifufuliwa. Angalia usambamba kati ya'roho’ ya Kristo na'mwili’ wake. kama mwili wake "haukuachwa kuzimu" ni kudokezwa kuwa alikuwako huko kwa kipindi, yaani, siku tatu ambazo mwili wake ulikuwamo kaburini. Kama Kristo alikwenda'kuzimu’ uwe ushahidi wa kutosha kwamba sio sehemu wanako kwenda wabaya.

Watu wote wabaya na wazuri wanakwenda'Kuzimu’ yaani kaburini. Hivyo Yesu "Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya" (Isa. 53:9) kwa kufuatana na mstari huu, ipo mifano mingine mingi ya watu wenye haki kwenda kuzimu, yaani kaburini. Yakobo alisema ya kwamba "nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu (kaburini) …. Akamlilia" Yusufu (Mwa. 37:35).

Ni moja ya mambo ya awali ya Mungu ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi ni mauti (Rum 6:23;8:13;Yakobo 1:15). Hapa kwanza tumeonyesha mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu kabisa. Dhambi husababisha kuangamia kabisa, sio kuteswa milele (math. 21:41;22:7; Marko. 12:9; Yakobo 4:12), hakika kama watu walivyoangamia kwa gharika (Luk. 17: 27, 29), Kama waisraeli walivyokufa jangwani (1 Kor. 10:10). katika sehemu zote hizi watenda dhambi walikufa kuliko waliteswa milele. Basi haiwezekani kwamba wabaya wanaadhibiwa wakiwa na fahamu kwa mateso na kuona.

Vile vile tumeona kuwa Mungu hahesabu dhambi - au kutuweka katika taarifa ikiwa hatujui neno lake (Rum 5:13). Walio katika nafasi hii watasalia wakiwa wafu. Walio kwisha jua matwaka ya Mungu watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi. Ikiwa wabaya adhabu wanayopata itakuwa ni kifo, kwa sababu hii ni hukumu kwa ajili ya dhambi. Kwa sababu hii baada ya kuja mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, wataadhibiwa na kisha kufa tena, kubaki katika kifo milele. Hii itakuwa ni'Mauti ya pili’ iliyosemwa katika ufu. 2:11; 20:6. Watu hawa walikuwa wamekufa mara ya kwanza, kifo cha kutokuwa na ufahamu kabisa. Watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi, na kisha kuadhibiwa na mauti ya pili, ambayo, kama mauti yao ya kwanza, hawatakuwa na ufahamu kabisa. Hii itadumu milele.

Ni katika maana hii ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi ni ya'milele’, katika hiyo haitakuwa na mwisho mauti yao. Kubaki wafu milele ni adhabu isiyo na mwisho. Mfano wa Biblia kutumia aina hii ya maelezo yanapatikana katika K/Torati 11:4. Huu unaeleza Mungu akiwaangamiza mara moja Jeshi la Farao katika Bahari ya shamu milele, maangamizi yanayoendelea ni kama hasa jeshi hili halikurudia tena kuwasumbua Israeli, "alivyowafunikiza na maji ya Bahari ya Shamu …….. alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo".

Hata katika nyakati za awali za Agano la Kale waamini walielewa kwamba kutakuwa na ufufuo siku ya mwisho, ambapo waovu wanaowajibika watarudi kaburini. Ayu. 21:30,32 yupo wazi sana: "Kwamba mwovu …… na kuongozwa nje (Yaani kufufuliwa) katika siku ya Adhabu ….. pamoja na hayo atachukuliwa (kwenda) kaburini". Moja ya mifano ya mahubiri kuhusu kurudi kwa Kristo na hukumu inazungumzia wabaya'Kuchinjwa’ mbele yake (Luk. 19: 27). Mfano huu ni shida kufaa katika wazo la wabaya wanaishi milele katika hali ya kuwa na fahamu daima wakipokea mateso. Kwa vyovyote hii itakuwa ni adhabu isiyo na maana - mateso ya milele kwa matendo ya miaka 70. Mungu haoni raha kuwaadhibu watu wabaya; basi inategemewa kuwa hatawapa adhabu isiyo na mwisho. (Ezek. 18:23, 32; 33:11; 2 Pet. 3:9).

Ufalme wa Kikristo ulioiacha imani mara nyingi unajumuisha'kuzimu’ na wazo la moto na mateso. wazo hili hutofautiana vikali na mafunzo ya Biblia kuhusu kuzimu (kaburi). "Kama kondooo wamewekwa kwenda kuzimu (kaburini); na mauti itawachunga" (Zab. 49:14) inadokeza ya kuwa kaburi ni mahala pa usahaulifu kwenye utulivu. Mbali ya roho ya Kristo, au mwili kuwa kuzimu kwa siku tatu, haukuachwa uoze (Mdo. 2:31) isingewezekana kama kuzimu ni mahala pa moto.

Ezek. 32: 26- 30 inatoa picha ya mashujaa wa vita wa mataifa yaliyowazunguka, wanalala kwa amani katika makaburi yao: "Mashujaa wao ….. walioanguka (katika vita) walioshuka kuzimu pamoja na silaha zao za vita: ambazo wameweka panga chini ya vichwa vyao ….. wamelala ….. pamoja nao washukao shimoni"Hapa tunatajiwa desturi za mashujaa kuzikwa na silaha zao na kukilaza kichwa cha maiti juu ya upanga wake. Lakini haya ni kueleza'Kuzimu’ - kaburi. Hawa watu mashujaa bado wanalala kuzimu (yaani, kaburini) ni shida kusaidia wazo la kuwa kuzimu ni sehemu ya moto.

Vitu vya mwili (kwa mfano, mapanga) kwenda sehemu moja "kuzimu" kama watu, ikionyesha kwamba kuzimu sio uwanja wa mateso ya kiroho. Hivyo Petro alimwambia mtu mwovu, "Fedha yako na ipotele mbali pamoja nawe (mdo. 8:20) Taarifa ya yaliyompata Yona yanapinga hili. Akiisha mezwa hai na samaki mkubwa, "Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki akisema, Nalimlilia Bwana …. Katika tumbo la kuzimu naliomba" (Yona. 2:1,2).'Tumbo la kuzimu’ hili ni sambamba na hilo la nyangumi. Tumbo la nyangumi kweli palikuwa ni'mahala pa uficho’ ambayo ndiyo maana ya neno msingi'Kuzimu’ lililotafsiriwa'kaburi’ Ni wazi haikuwa ni sehemu ya moto, Yona alitoka nje ya "tumbo la kuzimu" hapo nyangumi alipomtapika. Jambo hili lililenga mbele kwenye ufufuo wa Kristo toka'kuzimu’ (kaburini) - ona Mathayo 12:40.

MOTO ULIOELEZWA KWA MANENO YA MFANO

Walakini, Biblia mara nyingi inatumia mfano wa moto wa milele ili kuonyesha hasira ya Mungu kwa dhambi, ambayo itasababisha kuharibiwa kabisa mtenda dhambi kaburini. Sodoma iliadhibiwa na "moto wa milele" (Yuda. 7), yaani iliadhibiwa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wa wakazi. Leo mji umo katika maangamizi, umezama chini ya maji ya bahari ya chunvi, haumo kwa namna yoyote katika moto sasa, ambao ni wa muhimu tukitaka kuelewa'Moto wa Milele’ katika hali halisi. Vivyo hivyo Yerusalemu ilitishiwa na moto wa milele wa hasira ya Mungu, kwa ajili ya dhambi ya Israeli: "Kama hamtaki ….. basi nitawasha moto mlangoni mwake nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazima" (Yeremia 17:27). Yerusalemu ukiwa umetabiriwa kuwa mji mkuu wa ufalme ujao (Isa. 2:2 -4; zab. 48: 2), Mungu hakuwa na maana sisi tusome jinsi mstari ulivyo. majumba ya Yerusalemu yaliteketezwa hadi chini kwa moto (2 Fal. 25:9), Lakini moto ule haukuendelea milele.

Kama hivi, Mungu aliiadhibu nchi ya Edomu kwa moto ambao "Hautazimwa mchana wala usiku; moshi wake utapaa milele: tangu kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa; ….. bundi na kunguru watakaa huko ….. miiba itamea majumbani mwake " (Isa. 34:9 -15) Kwa kuwa wanyama na mimea walikuwa wawepo katika nchi iliyoharibiwa ya Edomu, Lugha ya moto wa milele inabidi iwe ni kutaja hasira ya Mungu na kuteketezwa kabisa sehemu yake, kuliko kuelewa kwa maneno halisi.

Mafungu ya maneno ya Kiebrania na kiyunani yaliyotafsiriwa "milele" maana yake iliyo halisi ni "muda mrefu" Wakati mwingine huu unatajwa wakati halisi usio na mwisho kwa kuwa mkubwa, kwa mfano muda wa ufalme, lakini sio daima. Mara kwa mara hasira ya Mungu kwa dhambi ya Yerusalemu na Israeli imefananishwa na moto: "Hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa (Yerusalemu) …… nayo itateketea, isizimike" (Yer. 7:20; mifano mingine inajumuisha omb. 4:11 na 2 Fal. 22:17).

Moto pia umeunganika na hukumu ya Mungu kwa dhambi, hasa Kristo akirudi: "kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi na watendao uovu, watakuwa makapi, na siku ile inayokuja itawateketeza" (Malaki. 4:1). wakati makapi au hata mwili wa binadamu, ukiungua kwa moto, unakuwa vumbi. haiwezekani kwa kitu chochote, hasa mwili wa binadamu kuungua milele. Lugha ya'moto wa milele’ basi hauwezi kutajwa kuwa mateso halisi ya milele. Moto hauwezi kudumu milele kama hauna cha kuunguza. ifahamike ya kuwa'Kuzimu’ nayo'inatupwa katika ziwa la moto (Ufu. 20:14). Hii inaonyesha ya kuwa kuzimu si mahala pamoja kama'Ziwa la moto’ hili linamaanisha maangamizo kamili. kwa namna ya mfano wa kitabu cha ufunuo, tumeambiwa ya kwamba kaburi litaharibiwa kabisa, kwa sababu mwishoni mwa Millenia (Miaka elfu) mauti haitakuwepo tena.

JEHANAMU

Katika Agano Jipya yapo maneno mawili ya Kiyunani yaliyotafsiriwa "hell" - kuzimu - Kiyunani'Hades’ ni maana moja na neno la Kiebrania'Sheol’. Hivyo kwa Kiebrania'shoel’, kiyunani'Hades’, kiingereza'hell’ ndipo tukapata neno letu kwa kiswahili'Kuzimu’ ambalo tumelijadili awali'Gehanamu’ ni jina la shimo panapomwagwa taka ambalo lilikuwa nje ya Yerusalemu, mahala uchafu wa kutoka mjini uliunguzwa.. Shimo hili la taka taka ni mfano mmoja na mingi ya miji inayoendelea siku hizi (k.m. mlima wa moshi, ulio nje ya manila nchini Ufilipino.) likiwa ni jina maalumu la mahali - likaachwa bila kulifasiri kwa jina'Gehanamu’ kuliko kutafsiri kuwa'Kuzimu’'Gehanamu’ ni Kiaramu sawa na Kiebrania "Ge -ben -Hinnon’. Hili lilikuwa karibu na Yerusalemu (Yoshua. 15:8). Na katika kipindi cha Kristo likawa ni dampo la taka za mji. Miili ya wahalifu waliokufa ilitupwa kwenye moto uliokuwa unawaka siku zote humo, hivyo Gehanamu ukawa ni mfano wa kuangamizwa kabisa na kukataliwa.

Tena, maana inabidi ieleweke ya kuwa kilichotupwa kwenye moto huu hakikusalia humo milele - miili ilioza na kuwa vumbi. "Mungu wetu (atakuwa) moto ulao" (Ebra. 12:29) siku ya hukumu; moto wa hasira yake kwa dhambi itawala watenda dhambi kwa kuangamia kuliko kuwaacha wameunguzwa huku bado wakiwa hai. Wakati wa hukumu za Mungu zilizopita kwa watu wake wa Israeli kwa mkono wa Wakaldayo, Gehanamu ilijawa na miili ya waliokufa ya watenda dhambi kati ya watu wake Mungu (Yer. 7:32,33).

Kwa jinsi ya uhodari Bwana Yesu aliyaweka yote mambo haya pamoja ya Agano la Kale kwa kulitumia hili neno'Gehanamu’. mara nyingi alisema ya kuwa wale wanaokataliwa kwenye kiti cha hukumu akirudi watatupwa Gehanamu (Yaani'kuzimu’), katika moto usiozimika; ambako funza wake hawafi (Marko. 9: 43, 44) Gehanamu iliweza kufikirishwa katika akili ya Wayahudi mambo ya kukataliwa na kuharibiwa mwili, tumeona kuwa moto wa milele ni neno lililotumika kwa namna ya kawaida linaloonyesha hasira ya Mungu juu ya dhambi, na kuwaangamiza wabaya kwa mauti.

Katika kutaja "ambamo funza hawafi", ni dhahiri sehemu ya msemo usiotumika kwa namna ya kawaida ikiwa ni mamoja na kuangamiza kabisa - haidhaniwi kuwa kunaweza kuwepo funza halisi ambao hawatakufa. Ukweli ni kwamba Gehanamu palikuwa ni sehemu ya adhabu zilizopita kwa wabaya miongoni mwa watu wa Mungu, Zaidi ya hayo Kristo anaonyesha namna ijayo kutumia mfano huu wa Gehanamu.


  Back
Home
Next